NILIOGELEA BAHARINI YA DHAMBI
1.
Niliogelea baharini ya dhambi,
nilisumbuka na kuteseka sana.
Sikujua kwamba, ninaye mpenzi,
(Nasikujua kunaye aliye upande wangu) x2
Sasa ninajua, ninaye Mpenzi,
anayeshughulika ninaposumbuka,
Unifikiria usiku na mchana,Na Nimejua
Ewe Bwana uko upande wangu x2
2.
Nilichoka sana, na kilichonichosha,
ni cha majuto kama maji ya kikapu.
Yesu kaniona, kanihurumia,
(Kaniambia kunacho nilichokuwekea) x 2
3.
Kapu la shetani niliacha pale,
ndani hakuna kilichotokea chote.
Kazi iliyo ngumu, kanipa shetani
(Eti na mwisho ni moto wa milele) x 2
4.
Ninafurahia huduma ya injili,
Nimefunguliwa, baharini ya dhambi.
ni kama ndama aliye malishoni,
(Eti na mwisho ni uzima wa milele) X2
1.
Niliogelea baharini ya dhambi,
nilisumbuka na kuteseka sana.
Sikujua kwamba, ninaye mpenzi,
(Nasikujua kunaye aliye upande wangu) x2
Sasa ninajua, ninaye Mpenzi,
anayeshughulika ninaposumbuka,
Unifikiria usiku na mchana,Na Nimejua
Ewe Bwana uko upande wangu x2
2.
Nilichoka sana, na kilichonichosha,
ni cha majuto kama maji ya kikapu.
Yesu kaniona, kanihurumia,
(Kaniambia kunacho nilichokuwekea) x 2
3.
Kapu la shetani niliacha pale,
ndani hakuna kilichotokea chote.
Kazi iliyo ngumu, kanipa shetani
(Eti na mwisho ni moto wa milele) x 2
4.
Ninafurahia huduma ya injili,
Nimefunguliwa, baharini ya dhambi.
ni kama ndama aliye malishoni,
(Eti na mwisho ni uzima wa milele) X2
