MAISHA YANGU MIMI NI MAFUPI
1
Maisha yangu mimi ni mafupi sana,
Yapita kama umande litokapo jua,
Yapita kama kivuli jua lituapo,
Mimi ni msafiri duniani hapa x 2
Nikiwa nayo mali bila Yesu bure,
Heshima madaraka bila Yesu bure.
Mauti yaningoja, kama vile Mamba,
Awindavyo Mawindo katika bahari x 2
2
Magonjwa yaningoja kama vile vumbi,
Njaa Vita Ajali vinapiga hodi.
Yesu ananishi tengeneza mambo,
Nisije nikapotea katika giza x 2
3
Heri kuchagua jina lililo jema,
La Yesu Mkombozi aliyetufia,
Utapata nguvu za kushinda maovu,
Kung’ang’ana na anasa mwisho kupotea x 2
1
Maisha yangu mimi ni mafupi sana,
Yapita kama umande litokapo jua,
Yapita kama kivuli jua lituapo,
Mimi ni msafiri duniani hapa x 2
Nikiwa nayo mali bila Yesu bure,
Heshima madaraka bila Yesu bure.
Mauti yaningoja, kama vile Mamba,
Awindavyo Mawindo katika bahari x 2
2
Magonjwa yaningoja kama vile vumbi,
Njaa Vita Ajali vinapiga hodi.
Yesu ananishi tengeneza mambo,
Nisije nikapotea katika giza x 2
3
Heri kuchagua jina lililo jema,
La Yesu Mkombozi aliyetufia,
Utapata nguvu za kushinda maovu,
Kung’ang’ana na anasa mwisho kupotea x 2
